Bunge la nchini Zimbabwe limepitisha sheria yenye utata ambayo inalenga kuwaadhibu raia wasioonyesha uzalendo, hatua ambayo kisheria inakinzana na ahadi ya Rais Emmerson Mnangagwa aliyotoa ya watu kuwa huru zaidi.

Chama tawala cha Rais Mnangagwa, ZANU-PF, kilitumia wingi wa wabunge wake kupitisha muswada huo mpya wa marekebisho ya Sheria ya Jinai (Codification and Reform) 2022 unaojulikana kama muswada wa uzalendo.

Sheria hiyo, ambayo imekuwa ikitumika tangu uchaguzi wa 2018 ilipitishwa siku iyo hiyo ambapo rais huyo mwenye umri wa miaka 80 alitangaza Agosti 23 kuwa tarehe ya uchaguzi mkuu. Uchaguzi huo unasubiriwa kwa hamu kubwa nchini humo.

Taarifa ya Baraza la Mawaziri mwaka 2022 ilisema: “Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Makosa ya Jinai (Mswada wa Marekebisho ya Kanuni na Marekebisho, 2022, unaongeza vifungu vya Sheria ya Makosa ya Jinai katika masuala yanayohusiana na mamlaka ya nchi hiyo kupitia kuharamisha mienendo ambayo inadhoofisha mamlaka ya Zimbabwe, utu, uhuru na maslahi ya taifa.”

Serikali yaanisha vipengele kuhamasisha utunzaji wa Mazingira
Wizara yapewa kibali kuajiri Watumishi sekta ya Afya