Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya imeteketeza jumla ya hekari 101 za mashamba ya bangi sawa na kiasi ya kilo 550 za bangi mbichi pamoja na magunia 482 ya aina hiyo ya dawa za kulevya katika eneo la Kisimiri juu kata ya Uwalu, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, kufuatia agizo la Rais Dkt. Samia la kufanya operesheni nchi nzima ili kuhakikisha dawa za kulevya zinatokomezwa Nchini.

Akizungumza operesheni hiyo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo amesema Mamlaka kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama itaendelea kufanya operesheni za mara kwa mara katika maeneo hayo, ili kuhakikisha bangi inatokomea kabisa mkoani humo.

Amesema, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa ameelekeza kufanyika kwa utafiti kujua ni mazao gani mbadala yanaweza kulimwa katika maeneo hayo, ambayo yamekithili kwa kilimo cha dawa za kulevya, ili wananchi wa maeneo husika waweze kupewa mbinu mbadala za kulima mazao mbalimbali ya chakula na biashara badala ya kuendelea na kilimo cha bangi.

“Elimu juu ya athari za biashara na matumizi ya dawa za kulevya itatolewa kupitia shule za msingi na sekondari. Hii inafanyika kufuatia agizo la Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Jesnista Mhagama kuitaka Mamlaka kushirikiana na wadau kutoa elimu katika maeno hayo.”

Kwa upande wake, Afisa kilimo Kata ya Uwelu, Samwel Parangyo utafiti uliofanywa na Wizara ya Kilimo kupitia kituo cha utafiti wa kilimo cha TARI Tenguru, umebaini kuwa yapo mazao yanayostawi katika maeneo hayo kama vile pareto, karoti na viazi mviringo na kuwa mbadala wa zao haramu la bangi.

Operesheni hiyo imefanyika ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama kutoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini kwa mwaka 2022 ambapo katika taarifa hiyo alitaaja mikoa inayojihusisha na kilimo cha Bangi kwa kiasi kikubwa, Mkoa wa Arusha Ukiwa kinara ukifuatiwa na Mikoa na Iringa, Morogoro na Manyara.

Abdallah Kibadeni aishauri Simba SC 2023/24
Benzema ajiweka njia panda Real Madrid