Mshambuliaji wa Ufaransa Karim Benzema anafikiria hatima yake Real Madrid baada ya kupokea ofa nono ya kuhamia Saudi Arabia, chanzo kilisema.

Benzema mwenye umri wa miaka 35, alipewa ofa ya mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Euro milioni 400, Januari, chanzo hicho kilisema ikiwa ni mkataba sawa na Cristiano Ronaldo aliyejiunga na Al Nassr baada ya kuondoka Manchester United.

Mshindi huyo wa Ballon d’Or 2022 alifikia makubaliano na Madrid mapema mwezi huu kuongeza mkataba kwa mwaka mmoja zaidi.

Hata hivyo, hali imebadilika katika wiki za hivi karibuni, na mshambuliaji huyo anafikiria ofa hiyo ya Saudia.

Madrid ilifanya vibaya katika msimu wa mwaka 2022-23 baada ya kushindwa kushinda na Barcelona katika mbio za kuwania taji la La Ligi na ikijikuta ikitolewa katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa kipigo kizito kutoka kwa Man City.

Benzema amekuwa akikabiliwa na maumivu msimu wa mwaka 2022 katika fainali za Kombe la Dunia, ambako Ufaransa ilimaliza ya pili nyuma ya Argentina.

Mamlaka yateketeza hekari 101, Magunia 482 ya Bangi
TFF yatoa kauli kifo cha shabiki Uwanja wa Mkapa