Uongozi wa Mtibwa Sugar Umeweka hadharani kuwa lengo lao ni kushinda mechi zao zote mbili zilizobakia za Ligi Kuu Bara kwa kuwa huu ndiyo muda wao wa kufanya hivyo.

Uongozi huo umeongeza kuwa wanataka kuanza kufanya hivyo kwenye mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar ambao ni wa dabi kwao na utapigwa Juni 6, Uwanja wa Manungu, Morogoro.

Afisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema: “Kikosi kinaendelea na maandalizi kwa ajili ya dabi hii ya sukari ambayo naamini itakua mechi ngumu sana kutokana na ubora wa wapinzani wetu.

“Tunahitaji kushinda mechi zetu zote zilizosalia msimu huu, huo ndo mkakati wetu wa kwanza kabisa kwa hiyo kwa njia yoyote ile lazima tupate ushindi mbele ya Kagera.”

Aliyevua nguo madhabahuni atoa sababu, akamatwa
Erling Haaland: Tunalitaka taji la Ulaya