Watu 26 wamefariki dunia katika kipindi cha wiki moja nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika jimbo la Beni, kivu ya Kaskazini.
Kwa mjiibu wa Gavana wa jimbo hilo, Julien Paluku amesema kuwa, serikali ya mkoa imetangaza hali ya tahadhari katika jimbo la Beni na vitongoji vyake ili kuzuia ugonjwa huo usiendelee kusambaa.
Aidha, amesema kuwa serikali tayari inazo dawa za chanjo, lakini imeomba washirika wa afya duniani ikiwemo shirika la afya duniani (WHO) kuendelea kuwasaidia katika kukabiliana na mlipuko huo mpya wa Ebola.
Hata hivyo, Ebola imetokea kivu kaskazini, wiki moja baada ya serikali ya DRC kutangaza kuwa ugonjwa huo uliojitokeza mwezi Mei katika jimbo la Equateur na ulizimwa baada ya kuuwa watu zaidi ya 30.