Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema asilimia saba ya Watanzania wanaishi na ugonjwa wa figo ambao ulihusishwa na shinikizo la juu la damu, ugonjwa wa kisukari na maambukizi ya VVU na UKIMWI.
Dkt. Mollel ameyasema hayo kwa niaba ya Serikali baada ya Mbunge wa viti maalum, Asia Abdukarimu Halamga kutaka kufahamu hali ya ugonjwa wa figo nchini.
Amesema, “naomba nitoe rai kwa wananchi kupima figo mara kwa mara kwani kuchelewa kutambua tatizo la figo madhara yake ni makubwa na gharama ya matibabu yake ni kubwa sana.”
Hata hivyo, mapema wiki hii Serikali ilisema mbele ya Bunge kuwa ina mpango wa kupunguza gharama za usafisahi figo kutoka Shilingi 350,000 hadi Shilingi 90,000.