Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali, kushirikiana na makampuni ya mawakala katika nchi husika kufanikisha azma ya kuwaleta watalii milioni tano ifikapo mwaka 2025.

Mchengerwa ametoa wito huom jijini Arusha, wakati wa mkutano maalum wa kibiashara kati ya makampuni makubwa ya watalii toka nchini China na wadau wa utalii nchini, akiambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Anderson Mutatembwa.

Amesema, anampongeza Balozi wa Tanzania nchini China kwa kushirikiana na wadau wengine kuratibu ujio wa mawakala hao na kutoa wito kwa mabalozi wengine kuiga mfano huo kwani nchi hiyo ni soko la kimkakati la utalii kwa Tanzania.

Aidha, Waziri Mchengerwa ameongeza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania na Ubalozi wa Tanzania nchini China wameandaa program maalum hii inayolenga kuwavutia watalii wengi kutoka China kuja kutembelea Tanzania.

Program hiyo itawasaidia watalii kutoka China kufurahia utalii wa Tanzania, pia kuratibu safari za kitalii ikiwa ni mwendelezo wa program ya Royal Tour iliyoasisiwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Mbeya City kutia mchanga pilau la Ubingwa?
Kashfa Sukari yenye sumu, Vigogo 27 wasimamishwa kazi