Zaidi ya Shilingi 972.076 Milioni, zimetengwa kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa Stendi mpya ya Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, itakayojengwa kwa siku 184 kuanzia hapo jana Oktoba 16, 2023 hadi April 15 2024 huku Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima akitaka ujennzi uendelee kwa amani na isiwe chanzo cha kuweka watu gerezani.

Akizungumza wakati wa makabidhiano na Mkandarasi Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Hamid Njovu amesema kwa awamu ya kwanza itahusisha eneo la awali la Stendi pamoja na uzio, maegesho ya magari, vibanda vya walinzi, sehemu ya kuingia na kutoka, Abiria kupumzika wakati wakisubiri magari na Maliwato ambapo katika awamu ya pili ya mradi huo litajengwa jengo la Bilioni mbili.

Awali, akizungumza katika eneo hilo Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima amewaomba Wananchi kutoa ushirikiano na kumuachia eneo hilo mkandarasi aendelee na ujenzi huku akitumia furusa hiyo kama mwenyekiti wa usalama wa Wilaya kutaka ujenzi huo uendelee kwa amani na sio stendi hiyo itumike kuweka watu Gerezani.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Wakili Stephano Byabato ambaye ni Naibu Naziri wa Mambo ya nje alikuwa mgeni rasimi katika hafra hiyo amewahakikishiwa waliokuwa wakifanya biashara zao kweye eneo hilo endapo ujenzi utakamilika watarejea kumalizia mikataba yao.

Utoaji wa ajira uzingatie usawa kijinsia - Kairuki
Wanafunzi acheni matumizi ya simu shuleni - ACP Mallya