Imeelezwa kuwa maaskofu wa kanisa katoliki, Amerika ya kusini wamepitisha pendekezo la kuwa na mapadri waliooa.
Maaskofu hao walio katika ukanda wa kusini mwa bara la Amerika wamependekeza baadhi ya wanaume waliooa kuruhusiwa kufanya kazi za upadri.
Pendekezo hilo limepitishwa kura za maaskofu 128 dhidi maaskofu 41 waliokataa, ambapo inasubiriwa idhini kutoka kwa papa francis ili kurasimisha pendekezo hilo.
Aina hiyo ya mapadri itaruhusiwa katika nchi ambazo zimethibitika kuwa na uhaba mkubwa wa mapadri, hivyo maaskofu waliopiga kura wanaamini nilazima Papa atauthibitisha utaratibu huo.
Nchi hizo ni Bolivia, Brazil, Colombia, Ecuador, French Guiana, Guyana, Peru Suriname, na Venezuela.