Ukraine imezidungua ndege zisizokuwa na rubani 45 za Urusi, wakati taifa hilo linaloungwa mkono na mataifa ya magharibi lilipokuwa likijiandaa kuukaribisha mwaka mpya 2023.

Jeshi la anga nchini humo limesema kwamba Moscow ilishambulia mji mkuu Kyiv na miji mingine kwa makombora na ndege zisizokuwa na rubani zilizotengenezwa na Iran.

Jeshi hilo limesema ndege 13 kati ya hizo zilidunguliwa mwishoni mwa mwaka 2022 na nyingine 32 katika mwaka huu 2023.

ndege isiyo na rubani (drone)

Hata hivyo mamlaka nchini humo hazijaweka wazi kama ndege hizo zimeleta madhara.

Baada ya majeshi ya Urusi kufurushwa katika maeneo iliyoyatwaa nchini Ukraine, mwezi Oktoba Moscow ilianza kuelekeza mashambulizi yake kwenye miundombinu muhimu ya Ukraine hususani ya umeme na kuwaacha mamilioni gizani na kwenye baridi.

TRA yavunja rekodi 2022
Mataifa nane Afrika kufanya uchaguzi 2023