Polisi imesema Watu kumi wamefariki, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya Lori walilokuwa wakisafiria kupinduka kufuatia kubeba mizigo kupita kiasi na hali mbaya ya barabara.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo la DRC, imeeleza kuwa Lori hilo aina ya Mercedes Benz liliondoka katika soko la Kiziba lililopo katika eneo la Shabunda barabara ya kuelekea Mwenga, Mkoa wa Kivu Kusini.

Moja ya ajali ya Lori kupinduka kusini mwa nchi ya DRC. Picha ya

Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama katika mkoa wa Kivu Kusini, Théophile Kiluwe Migo amesema “Ajali hii imesababisha vifo vya watu kumi na wengine kujeruhiwa, waathriwa wote ni abiria wanaume sita na wanawake wanne.”

Aidha, Waziri Migo amefafanua kuwa, “Kupakia mizigo kupita kiasi na ubovu wa barabara ndio chanzo cha ajali hii hapa DRC, nchi ina kilomita za mraba milioni 2.3 na barabara zinazopitika ni chache, ajali nyingi zinaripotiwa, na mara nyingi hasara ni kubwa.”

'FOA' ya Diamond album bora ya mwaka AEAUSA
Dkt. Mwinyi apita njia moja na Dkt. Samia