Takriban watu tisa wamefariki ,na wengine ambao idadi yao haikuweza kujulikana mara moja kujeruhiwa baada ya kutokea mkanyagano wakati wa shamrashamra za sherehe ya mwaka mpya jijini Kampala nchini Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi nchini Uganda, imesema baadhi ya waliofariki ni watoto waliokuwa wakihudhuria hafla hiyo ya burudani ndani ya jumba lenye maduka kando ya barabara kuu ya Kampala kuelekea Entebbe liitwalo Freedom City Mall.

Jumba lenye maduka lililopo kando ya barabara kuu ya Kampala – Entebbe, Freedom City Mall. Picha ya DN.

Taarifa hiyo, imeeleza kuwa umati ulijitokeza kutazama onyesho la fataki majira ya  usiku uliingia katika kadhia ya mkanyagano uliopelekea wengi wao kujeruhiwa na baadhi kufariki papo hapo na Hospitalini.

Aidha, Polisi inasema uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea ili kubaini kilichotokea katika maonesho hayo ya fataki ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2023 yaliyoruhusiwa katika Taifa hilo.

Dkt. Mwinyi apita njia moja na Dkt. Samia
Picha: Mataifa yalivyoupokea mwaka 2023