Watu sita wamefariki Dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya mabasi mawili kugongana uso kwa uso kwenye Barabara kuu ya Ntungamo-Kabale magharibi mwa Uganda.

Ajali hiyo ya Desemba 29, 2022 ilitokea eneo la Hakabira juu ya kilima cha Rwahi katika halmashauri ya mji wa Rwahi, Wilaya ya Ntumgamo, huku chanzo chame kikidaiwa kuwa ni hali mbaya ya hewa.

Eneo la ajali katika kilima cha Rwahi uliopo Halmashauri ya mji wa Rwahi wilayani Ntumgamo. Picha ya Robert Muhereza.

Mashuhuda wa ajali hiyo, walisema majira ya saa kumi jioni, dereva wa basi la Volcano lenye namba za usajili wa nchini Rwanda alibadili njia na kuligonga basi hilo la Oxygen lenye namba za usajili wa nchini Kenya.

Basi hilo la Volcano, lilikuwa likitokea jijini Kampala likielekea mji mkuu wa Rwanda Kigali, wakati basi la Oxygen lilikuwa likisafiri kuelekea jijini Nairobi Kenya kutoka Kigali, huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigezi, SSP Ibrahim Saiga akisema ukungu wa asubuhi uliwafanya madereva wasionekane na kusababisha ajali hiyo.

TANROAD yatangaza kulifunga Daraja la Tanzanite
Salamu za Mwaka mpya kwa Watanzania