Sherehe za Miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambazo hufanyika Januari 12 kila mwaka zimefutwa na fedha ambazo zilizotengwa kwa ajili ya shughuli hiyo zitatumika katika mahitaji mbalimbali ya sekta ya elimu.

Uamuzi huo, umetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye amesema sherehe hizo zilipaswa kutumia kiasi cha shilingi 700 milioni.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Amesema, kiasi hicho cha pesa kilipunguzwa hadi kufikia shilingi 450 milioni ambazo serikali imezielekeza  kuongeza nguvu  kwenye sekta ya elimu eneo la madarasa, madawati, maabara na huduma nyingine.

Desemba 5, 2022 akiwa jijini Dodoma Rais Samia Suluhu Hassan naye Ali futa sherehe za Miaka 61 ya uhuru na kuagiza fedha zote kiasi cha shilingi milioni 960 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya shughuli hiyo zielekezwe katika ujenzi wa Mabweni wa shule nane za wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Gari lapinduka sokoni, 10 wafariki
Tisa wafariki kwa mkanyagano mkesha wa mwaka mpya