Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amewaonya raia wake dhidi ya mashambulizi zaidi ya Urusi katika siku chache zilizobakia za mwaka wa 2022.
Kupitia ujumbe wa video, Zelensky amesema vikosi vya Urusi vitajaribu kufanya hali kuwa mbaya zaidi na kusema tayari imepoteza kila kitu kwa mwaka huu.
Zelensky ambaye amekuwa akiungwa mkono katika vita hivyo na mataifa ya magharibi, amesema Urusi inajaribu kufidia hasara kwa kueneza propaganda baada ya mashambulizi ya makombora yaliolenga kwenye sekta ya nishati.
Aidha, amevishutumu vikosi vya urusi ambavyo viliua takriban watu 16 na kujeruhi wengine 64 katika mashambulizi ya mizinga huko Kherson, kusini mwa nchi hiyo siku ya Jumamosi Desemba 24, 2022.