Msanii anaefanya vizuri kwa sasa katika kiwanda cha muziki wa bongo fleva anaye iwakilisha A city na wimbo wa my life Dogo janja ”Janjaro hivi karibuni ameachia remix ya wimbo wake huo akiwa amewashirikisha mastaa wakubwa kutoka Uganda Radio na Weasel

DOGOO

Unaweza kudhani kuwa msanii huyu mwenye umri mdogo na jina kubwa aliridhika na mafanikio ya wimbo wa my life kabla Uongozi wake kumshauri kufanya huo na wasanii hao kutoka Uganda kumbe kwa upande wake ilikuwa tofauti.

”Nilikuwa natamani sana kufanya na G nako wimbo huu lakini kwa vile dereva wa mziki wangu ni uongozi waliposema Radio na Weasel sikuwa na ubishi Alhamdulillah umekuwa mkubwa kuliko nilvokuwa nautarajia” Alisema Janjaro wakati akipiga story na Dar24.

Akizungumzia suala linalolalamikiwa na wadau wa mziki kuwa wasanii ndio chanzo uadui kwa watayarishaji wa video, amesema msanii siku zote anaangalia biashara yake hivyo haoni tatizo kwa msanii kuhamisha kazi yake sehemu moja kwenda nyingine kama tu anatafuta ubora wa biashara yake.

Hata hivyo amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kupokea video hiyo ambayo itaachiliwa muda wowote mapema huku akisema jina la Mtayarishaji wa video litakuwa wazi mapema zaidi.

 

Pele Aingia Kwenye Mkumbo Wa Kumbembeleza Messi
Diego Costa Aomba Kuondoka Stamford Bridge