Gwiji wa soka duniani, Edson Arantes do Nascimento Pele amekua sehemu ya wadau wanaendelea kumtaka mshambuliaji Lionel Messi abadilishe mawazo ya kustaafu soka la kimataifa.

Pele amekua sehemu ya watu hao, baada ya kumtaka Messi kusahau yaliyopita na kujiona kama mkosefu mbele ya taifa lake, kutokana na mkwaju wake wa penati ambao uliota mbawa wakati wa mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya Copa America dhidi ya Chile uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita nchini Marekani.

Pele amemwambia Messi, kwamba ni mapema mno kwake kutangaza kustaafu soka, kutokana na umri wake kumruhusu kuendelea kuitumikia timu yake ya taifa ambayo inahitaji msaada mkubwan kutoka kwake.

Gwiji huyo ambaye anaendelea kuheshimika dunaini kote, amesema anaamini Messi alipandwa na hasira baada ya kuona imekua kama bahati mbaya kwa kushindwa kuisaidia Argentina kutwaa mataji tangu apoanza kuitumikia timu ya taifa ya wakubwa mwaka 2005.

Amesem ni vigumu kwa kila binaadamu kuamini kama kweli Argentina walishindwa kutwaa ubingwa wa kombe la dunia mwaka 2014, ubingwa wa Copa America mara mbili mwaka 2015 na 2016 wakiwa na mchezaji mahiri kama Lionel Messi, hali ambayo inaonyesha kumkereketa mshambuliaji huyo wa FC Barcelona.

“Ni Mapema mno kwake kufanya maamuzi ya kustaafu kuichezea Argentina, kwanza ukiangalia bado ana umri wa miaka 29 ambao unamruhusu kuendelea kucheza soka lake na kufikia mafanikio,

“Pili bado ana uwezo mkubwa wa kuwasaidia wengine na kuonyesha mfano kwa vijana ambao wanapenda kuwa kama yeye na kufikia lengo la kucheza katika timu ya taifa ya Argentina,

“Na tatu Lionel Messi ni mchezajia mbaye hachoshi kumtazama pale anapokua uwanjani akicheza na timu yake ya taifa ama klabu yake ya FC Barcelona, hivyo kama ataamua kukaa pembeni kwa maamuzi aliyoyatangaza ya kustaafu atakua amewanyima jambo fulani mashabiki wanaopenda kumfuatilia.” Alisema Pele

Lionel Messi alitangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa, saa chache baada ya kikosi cha Argentina kushindwa kutwaa ubingwa wa Copa Amarica, baada ya kufungwa na Chile kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Video: RC Makonda amepokea msaada mwingine Hospitali za Dar es salaam
Ukubwa wa ''My life Remix'' ni Tofauti na Nilivyoifikiria -Dogo Janja