Raia wa Zambia wamejitokeza kupiga kula siku ya leo, huku upinzani mkali upo kati ya chama cha Ruling Patriotic Front (PF)  kinachoongozwa na Rais Edger Chagwa  Lungu dhidi ya chama cha United Party for National Development (UPND) kinachoongozwa na Hakainde Hichilema.

Rais Edgar Lungu anawania kutawala kwa muhula wa pili huku akikabiliana na ushindani mkubwa kutoka kwa Hakainde Hichilema, mgombea wa chama kikuu ya upinzani nchini humo.

Ni mara ya tatu kwa kiongozi wa UPND Hichilema na kiongozi wa PF Lungu kukabiliana katika uchaguzi mkuu.

Katika uchaguzi mdogo wa mwaka 2015, ambao ulitokana na kifo cha marehemu Rais Michael Sata, Hichilema alishindwa na Lungu kwa tofauti ya kura 27,700.

  • Tanzania , Ethiopia kuendeleza uhusiano

Katika uchaguzi mkuu wa 2016 Hakainde alishindwa tena lakini akafanikiwa kuongeza idadi ya wafuasi waliompigia kura  hadi nusu. Alishindwa kwa karibu kura 13000 tu.

Hata hivyo Polisi na wanajeshi wanafanya doria nchi nzima katika vituo vya kupigia kura na idadi kubwa ya waangalizi wa kimataifa watakuwa wakifuatilia mchakato huo.

Huku wapiga kura wengi wakiwa wanataka hali ya uchumi kuboreshwa na fursa za ajira kupatikana. Tume ya uchaguzi nchini Zambia imehaidi uchaguzi wa uwazi na haki.

  • Uwanja wa ndege kugharimu bilion 35 Musoma
  • Huu ndo wito wa Waziri Gwajima kwa wananchi

Naibu Waziri aainisha manufaa ya anwani za makazi na postikodi
Mawasilino kuimarishwa mipakani, Tarime na Rorya kunufaika