Wakala wa usajili wa biashara na leseni – BRELA, imewataka wafanyabishara wakubwa, wakati na wadogo nchini kufuata sheria na taratibu zilizopo ikiwa ni pamoja na kurasimisha biashara zao, ili kuchangia pato la Taifa huku ikisema itawasaidia kupata mikopo kutoka katika taasisi za kifedha.
Rai hiyo imetolewa na Afisa leseni wa BRELA, Jubilae Muro wakati akizungumza na wanahabari katika maonyesho ya 10 ya Biashara na viwanda yanayofanyika mkoani Tanga na kuongeza kuwa wapo baadhi ya wafanyabishara wanaofanya kazi zao kinyume cha sheria.
Amesema, “tunawaomba wafanyabishara wote nchini wasajili biashara zao kwasababu kuna faida kubwa kwa kufanya hivyo kuliko kutokusajili a lakini pia kuna huduma zingine mfanyabishara ,mmiliki wa kiwanda au kampuni atashindwa kuzipata kwa kukwepa kusajili biashara yake kupitia BRELA.”
Muro ameongeza kuwa, “lakini hii pia itamsaidia kujenga uaminifu kwa wateja wake na wafanyabishara wengine na hata kwenye taasisi za kifedha ataweza kuhudumiwa kama atahitaji mkopo akiwa na leseni ya kibiahara vinginevyo anaweza kukosa huduma muhimu ambazo zinaweza kumleta maendeleo.”
Kwa upande wake Afisa usajili kutoka BRELA Julieth Kihwelu alisema kuwa mifumo hiyo ni mikuu na iliyo pendwa ambayo mwombaji anatakiwa kutumia kuwasilisha ombi lake huku akieleza wanatoa huduma ya kuwafundisha namna ya kutumia mfumo huo kuweza kujisajili.
Maonyesho hayo ya Biashara na Utalii na ya 10 kwa mwaka huu wa 2023, hufanyika kila mwaka jijini Tanga, yakihusisha Taasisi za Umma na Serikali yamebebwa na kauli mbiu ya ‘Kilimo , viwanda utalii na madini ndio msingi wa maendeleo ya kiuchumi.’