Mhubiri wa kanisa la Muungano Church for All Nations, Geoffrey Wanyama (83), maarufu kama ‘Nabii Yohana wa Tano’ amefika mbele ya maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), na polisi mjini Bungoma ili kuhojiwa kuhusu kanisa lake.

Hatua hiyo inajiri baada ya Kamanda wa Polisi Bungoma Francis Kooli kuzuru nyumbani kwake wiki hii na kumwagiza afike mbele ya maafisa kuhojiwa kwa kuandika Biblia yake yenye vitabu 93 kikiwemo cha Agnes, jina ambalo imebainika linafanana na la mmoja wa wake zake.

Mara baada ya kugojiwa, ‘Nabii Yohana wa Tano’ amedai Biblia anayotumia yenye vitabu 93 pamoja na amri 12 ni halali kwa sababu alikabidhiwa na Mwenyezi Mungu na kwamba hakuandika mwenyewe Biblia hiyo kama inavyodaiwa na watu.

Mhubiri huyo anahojiwa siku chache tu baada ya mhubiri mwingine wa kanisa la New Jerusalem Eliud Wekesa almaarufu Yesu wa Tongaren kuchunguzwa na kufikishwa mahakamani na hata hivyo, Yesu wa Tongaren aliachiliwa baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha madai dhidi yake.

Wazazi walindeni watoto - Gwajima
Bares: KMC waje kwa tahadhari Sumbawanga