Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Mohamed Abdallah ‘Bares’ amefunguka kuwa wamejipanga vizuri kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya KMC FC unaotarajiwa kupigwa Juni 6, katika uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa huku akitamba wanataka alama za wapinzani wao.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Prisons inashika nafasi ya nane ikiwa na alama 34.

Bares amesema: “Vijana wangu wapo vizuri kwa ajili ya mchezo huu, bado wanaendelea na mazoezi kubwa zaidi kwetu ni kupata ushindi wa alama tatu ili tuweze kujiweka kwenye sehemu salama zaidi kwenye msimamo.

“KMC nawafahamu vizuri kwa hiyo kama kocha najua niingie na mbinu gani kwenye mchezo huu ili tuweze kuwadhibiti wapinzani wetu na kupata ushindi ambao ni muhimu sana kwetu.”

Madai ya kuandika Biblia yake, Polisi wamhoji Nabii Yohana
Asensio huyooooooooo PSG