Wakati wowote ule tarajia kumuona winga Marco Asensio akitambulishwa ndani ya PSG kama mchezaji wa timu hiyo baada ya wawili hao kukubaliana juu ya nyota huyo kusaini klabuni hapo.

Asensio atajiunga na PSG kama mchezaji huru akitokea Real Madrid baada ya kukubali ofa ya timu hiyo na kuachana na Aston Villa ambao nao walionyesha nia ya kuhitaji huduma ya Mhispania huyo.

Nyota huyo anatarajiwa kutoa heshima zake za mwisho kwa mashabiki wa Real Madrid leo Jumamosi (Juni 03) kabla ya kuondoka klabuni hapo wiki ijayo na kwenda kuanzia maisha nje ya klabu hiyo ambayo amedumu nayo kwa muda mrefu.

Bares: KMC waje kwa tahadhari Sumbawanga
Zoezi uhamishiaji Wananchi Msomera halijasimama - Serikali