Uongozi wa Majogoo wa Jiji ‘Liverpool FC’ umekubali kuvunja Benki na kutoa kitita cha Pauni Milioni 60 kwa ajili ya kukamilisha usajili wa nyota wa RB Leipzig, Dominik Szoboszlaí baada ya kukidhi baadhi ya vipengele vya mkataba wake.

Huu unatarajiwa kuwa usajili wa pili kwa Liverpool katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi.

Mazungumzo baina ya pande hizo mbili yalishika kasi siku ya Ijumaa (Juni 30), saa chache kabla ya kifungu cha kutolewa kwa mchezaji huyo cha Pauni milioni 60 na timu hiyo ya Bundesliga kukamilika, huku Leipzig wao Wakikamilisha usajili wa mkopo wa msimu mzima kwa chipukizi wa Reds Fabio Carvalho.

Leipzig haikuwa na haraka ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, hasa baada ya kuachana na nyota wao Christopher Nkunku ambaye amejiunga na Chelsea na Josko Gvardiol akiwa anawindwa na Manchester City kwa uhamisho wa pesa nyingi mwezi huu, lakini Szoboszlai aliweka wazi alitaka nafasi hiyo ya kuhamia Anfield na kufanya kazi na Jurgen Klopp.

Akizungumzia uhusiano wake na Klopp, Szoboszlai mapema mwaka 2020 alinukuliwa akisema: “Ninampenda sana Klopp, jinsi anavyoweza kuwatia moyo wachezaji wake.”

“Hata kama hawana chochote, wanaweza kusimama na wachezaji wake wanaweza kufikia lolote. Kwangu mimi ndiye meneja bora zaidi duniani.”

Wapora mali za marehemu, wazirejesha bila kupenda
Matumizi ya Teknolojia: JKT liwekeze kwa Vijana - Dkt. Mpango