Jeshi la Marekani limedungua ‘kifaa’ kipya kwenye mwinuko juu ya Ziwa Huron, kikiwa ni cha tatu kuonekana angani na kuharibiwa ndani ya siku tatu na cha nne chini ya siku kumi kitu ambacho kinaziweka nchi za Marekani na Canada katika hali ya tahadhari.

Tukio hilo ni mwendelezo wa matukio ya ulipuaji wa vitu vya angani likiwemo puto la China lililodaiwa na Marekani kama ni kifaa cha kijasusi na ambacho kilidunguliwa na kombora Februari 4, 2023 baada ya kuruka juu ya anga la Marekani.

Mbunge wa chama cha Democratic wa jimbo la Michigan, Elissa Slotkin aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa, “kama tahadhari na pendekezo la amri ya kijeshi, Rais Biden ameagiza kwamba kitu kisichojulikana kiangushwe haraka.”

Mamlaka za usalama za Marekani zinasema kifaa cha kwanza kilichogunduliwa awali kilikuwa ni puto ambalo lilihodhiwa na jeshi la China kilichotumwa kuzifuatilia nchi zaidi ya 40 kwenye mabara matano, kikilenga kufanya ujasusi.

2023: Mwaka wa harakati za kisiasa barani Afrika
Bodi DAWASA yaridhishwa maendeleo mradi JNHPP