Usalama umeimarishwa hii leo jijini Nairobi wakati Rais Uhuru Kenyatta akitarajiwa kuapishwa kuiongoza Kenya kwa awamu ya pili.
Aidha, Kiongozi wa upinzani, Raila Odinga ambaye alisusia marudio ya uchaguzi ameitisha kufanyika kwa mkutano wa upinzani licha ya mkutano huo kupigwa marufuku.
Katika sherehe hizo za kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta, zinatarajiwa kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa kigeni akiwemo waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni na Rais wa Rwanda, Paul Kagame na Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.
Hata hivyo, Upinzani nchini humo umewataka wafuasi wake kususia sherehe hiyo na badala yake kukusanyika katika mkutano ili kuwakumbuka wafuasi waliouawa katika ghasia tangu uchaguzi wa mwezi Agosti.