Manchester City imefanikiwa kupata mataji matano ya Ligi Kuu ya England, mawili ya FA na manne ya EFL katika zama za Pep Guardiola na sasa itakuwa na nia ya kuongeza taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati leo Jumamosi (Juni 10) itakapocheza na Inter Milan mjini Istanbul nchini Uturuki.
Guardiola alishinda Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili akiwa na FC Barcelona lakini amejaribu mara sita katika mashindano hayo akiwa na Man City, ikiwa ni pamoja na kufungwa 1-0 na Chelsea kwenye fainali ya mwaka 2021.
Kocha wa Inter Milan Simone Inzaghi, hajawahi kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa akiwa mchezaji au kocha, lakini pia anawinda taji la tatu msimu wa 2022-23, baada ya kuiwezesha Inter kutwaa ubingwa wa Supercoppa Italiana na Coppa Italia.
Nathan Ake alirejea mchezaji wa akiba katika fainali ya Kombe la FA na kuwafanya Man City sasa kutokuwa na majeruhi yoyote kuelekea mchezo wa leo Jumamosi (Juni 10).
Kama Inter hawatakuwa na Dalbert (aliyeumia goti), kuna mashaka kama Henrikh Mkhitaryan (anayesumbuliwa na misuli) na Joaquin Correa (misuli) kama wataweza kucheza.
Milan Skriniar kwa upande wake, hajacheza tangu Machi kutokana na jeraha la mgongo.