Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi H. Chana kwa mamlaka amewateua wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI).
Balozi Chana amefanya uteuzi huo, chini ya Kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Utafiti wa Misitu Tanzania Na.5 ya Mwaka 1980, kinachompa mamlaka ya kuteua wajumbe hao.
Walioteuliwa ni Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi, Maendeleo ya Ufugaji Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Daniel Charles Pancras na Profesa wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Faustin Rweshabura Kamuzora.
Wengine ni Dkt. Zanifa Omary, Mhadhiri, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Mkurugenzi wa Fedha, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Beatrice Musa Lupi, Afisa Uratibu wa Utafiti Mkuu, Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH), Dkt. Hulda Gideon Mapunjo.
Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, John John Nchimbi, Wakili wa Serikali wa Mkoa wa Morogoro, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Adv. Xavier Masalu Ndalahwa na Dkt. Revocatus Petro Mushumbusi, Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) anakuwa katibu wa Bodi hiyo.
Uteuzi huo wa miaka mitatu kuanzia Januari 30, 2023 – Januari 31, 2026 unafuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kumteua Prof. Verdiana Grace Masanja kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI).