Watanzania wametakiwa kushiriki kwenda kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii, kwa lengo la kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kutangaza utalii.
Wito huo, umetolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Kata ya Mabwepande Jimbo la Kawe (UVCCM), Andrew Mashimba wakati akizungumza na vyombo vya habari.
Mashimba, amesema lengo la kuandaa matembezi hayo ya kwenda Sadaan ni kwa lengo la kumuunga mkono mama Samia katika jitihada zake za kutangaza utalii wa Nchi yetu.
“Sisi tukiwa vijana lazima tumuunge mkono mama na kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa hivyo uchaguzi umeisha na sasa Kazi Iendelee,” amesema Mashimba.
Naye Katibu wa UVCCM Mabwepande Ramadhani Kindamba amesema kuwa wamejipanga vizuri katika kuhakikisha jambo hili linatimia.