Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umesema kuwa licha ya sifa nyingi anazozipata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli lakini bado tatizo la rushwa lipo.
Kutokana na tatizo hilo, Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mbeya na Songwe, Aman Kajuna amemtaka Rais Magufuli kutumia nguvu kubwa kutokomeza tatizo hilo ambalo limekuwa ni sugu.
Kajuna ambaye aliongozana na mwenyekiti mwenzake wa mkoa wa Kagera, Yahaya Katema walikuwa wakizungumza kwa niaba ya wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM na walimsifu Rais kuwa amekuwa kiongozi wa mfano.
Aidha, pamoja na sifa hizo viongozi hao wametilia shaka suala zima la rushwa, kilimo na tatizo la maji ambalo wamesema kuwa matatizo hayo bado ni sugu hivyo anatakiwa kuyatilia maanani.
“Nikweli bado tunachangamoto kubwa katika baadhi ya maeneo kama tatizo la rushwa, kilimo na maji, kitu amabacho wananchi wengi hasa vijijini wamekuwa wakihangaika navyo, tunamuomba Rais Dkt. Magufuli atilie mkazo katika haya,”amesema Kajuna
-
BAVICHA walibipu jeshi la polisi, wasema maombi yako palepale
-
Msigwa amvaa Musukuma, amtaka aache kulalamika
-
Diwani amtaka Mbowe kumtafuta Dkt. Slaa
Kwa upande wake mwenyekiti wa mkoa wa Kagera, Yahaya Katema amesema kuwa kuna mambo mengi ambayo hayajatekelezwa lakini ni mapema sana kwa sasa kuweza kutoa majibu yaliyojitoshereza.