Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo amepiga marufuku uwindaji wa Panya unaofanywa na wananchi kwa kutumia njia ya kuchoma moto.

Akitoa agizo hilo, Wangabo amesema kuwa ikiwa sababu kuu ya kuwinda panya msituni ni kutafuta kitoweo basi wananchi hao hawanabudi ya kuanza kufuga kuku ili kupata kitoweo mbadala.

Katika kuhakikisha agizo la serikali la kila halmashauri kupanda miti milioni 1.5, kila mwaka, Wangabo amesema ni lazima vyanzo vyote vya uharibifu wa miti vidhibitiwe ambapo moja ya chanzo ni uwindaji panya kwa kuchoma misitu.

Ofisa aridhi na Maliasili wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga, Juma chande ndiye aliyetoa siri hiyo ya uharibifu wa misitu na kusisitiza kuwa ni utamaduni wa muda mrefu wa wakazi wa wilaya hiyo.

Aidha, maeneo yaliyotajwa kuathiriwa zaidi na uchomaji moto wa misitu kwa kufuata tamaduni hiyo ni vijiji vya Msanda, Muungano, Sandulula na Mpwapwa.

Hata hivyo, mkuu wa mkoa ametoa agizo kwa wakurugenzi wote wa halmashauri kuwasilisha mpango mkakati wa upandaji miti kwa kipindi cha mwaka huu, ikiwa ni pamoja na kubainisha idadi ya miti waliyonayo na mahali ilipo.

 

Video: Watetezi wa haki za binadamu waungana nchi nzima
WhatsApp yaweka zuio kutuma ujumbe zaidi ya mara tano