Mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva Tanzania na Afrika, Vanessa Mdee ametangaza rasmi kuacha muziki na kupumzika kwa muda kufanya kazi hiyo kutokana na matendo yaliyomo ndani ya tasnia.

Akizungumza kwenye kipindi chake cha redio mtandaoni (podcast) Vanessa amesema tasnia ya muziki imejaa mambo ya ajabu yasiyoaminika machoni pa watu.

“Kilichonifanya nichukue likizo kwenye muziki ilikuwa ni kuchagua maisha yangu na muziki unajua unapoingia kwenye tasnia watu wanakuambia upande mmoja tu wa mazuri na kusahau mabaya, kiukweli tasnia ya muziki imejaa mabaya mengi na ilibidi nichague kundelea kwenye ubaya au maisha yangu” amesema Vanessa.  

Na kusisitiza ”kwa wale wasanii waafrika ambao wanaotamani waishi the american dream ama wafike marekani wakafanikiwe huko waache hizo ndoto, kwasababu ni kugumu kina selena Gomez huko wako wengi na hawana nafasi kama unataka kung’aa ng’ara huko uliko ng’ara nyumbani”

Ikumbukwe kuwa kwa sasa Vanessa anaishi Atlanta nchini Marekani akiishi na mwenzi wake Rotimi ambaye ni muigizaji pia ni mwanamuziki.

Facebook yafuta matangazo ya kampeni za Trump yenye chuki
Hospitali ya Amana yarejesha huduma kama awali