Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametangaza kuwa huduma kwa wagonjwa wa kawaida katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dar es salaam, Amana zimerejea kama kawaida.

Ummy amesema uamuzi huo unatokana na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa wagonjwa wa COVID19 nchini hususan katika Jiji la Dar es salaam.

Amesema, “Serikali imerejesha rasmi huduma zote za Matibabu zinazotolewa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana na Wananchi wawe huru kwenda kupata huduma”

Hata hivyo, amebainisha kuwa Serikali inaendelea kusisitiza kuzingatiwa kwa Kanuni za Uthibiti wa maambukizi na kuwataka watu wote wanaokwenda katika Vituo vya kutoa huduma za Afya kuvaa barakoa za vitambaa, kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka na kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu.

Vanessa Mdee atangaza kuacha muziki, 'Umejaa mabaya mengi'
Wagonjwa mikoani kutibiwa MOI kwa mtandao