Katibu Mkuu wa (BAVICHA) Julius Mwita amesema kuwa kitendo cha, Edward Lowassa kwenda kukutana na Rais Ikulu siyo tatizo ila tatizo ni kumsifia kiongozi huyo wakati ambao kuna mambo mengi hayaendi sawa.
Ameyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari na kudai kuwa msimamo wa BAVICHA ni ule ambao umetolewa na Mwenyekiti wa chama chao kuwa kauli alizotoa Edward Lowassa kwa Rais ni maoni yake binafsi na si msimamo wa chama chao.
“Lowassa akiamua kurudi CCM sisi hatuwezi kuogopa bali tutamshukuru kwa kipindi chote amekaa na sisi na tutamtakia maisha mema kama ambavyo tumewatakia maisha mema viongozi wote waliondoka CHADEMA kwenda CCM kwa sababu Katiba ya nchi hii inampa uhuru mwananchi yoyote ama kuwa na chama au kutokuwa na chama, ukiamua kuwa na chama bado utaamua wewe uwe katika chama gani CHADEMA, TLP au chama kingine chochote siku ukiamua kutoka NCCR kwenda chama kingine hawawezi kukuzuia kutoka.” amesema Mwita