Ligi kuu ya soka ya England imeendelea, ambapo vinara wa Ligi Chelesa wamepambana na Middlesbrough na kuibuka na ushindi wa goli tatu kwa sifuri.

Magoli mawili ya Diego Costa na Marcos Alonso kipindi cha kwanza na goli la tatu la Nemanja Matic aliyefunga kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Stamford Bridge yameifanya Chelsea kuwa na point saba mbele ya wapinzani wao wa karibu Tottenham.

Chelsea wakiwa na michezo mitatu iliyosalia huenda wakatangaza ubingwa usiku wa ijumaa ya wiki hii endapo watafanikiwa kuvuka kihunzi vya West Brom katika uwanja wa West Bromwhichalbion.

Chelsea inayo nafasi moja tu kufikia kileleni mwa ligi baada ya kuichabanga timu ya Middlesbrough kwa bao tatu kiduarisho katika uwanja wa Stamford Bridge.

Antonio Conte aliwabugiza Middlesbrough kwa magoli baada ya kupokea pasi iliyotakata kutoka kwa Diego Costa, Marcos Alonso na Nemanja Matic, na huenda Chelsea watatawazwa kuwa vijogoo wa ligi kuu ya England endapo watafanikiwa kuvuka kihunzi katika uwanja wa West Bromwhichalbion siku ya ijumaa.

Prof. Muhongo aahidi neema kwa wachimbaji wadogo wadogo wa madini
?LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Mei 9, 2017