Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria  na Haki za Binadamu (LHRC), Hellen Kijo Bisimba amesema Serikali imeanza kazi vizuri ikiwa ni pamoja na kupambana na ufisadi, kuhakikisha Serikali ina wafanyakazi wanaojali kazi zao pamoja na utawala mzuri wa watendaji wa Serikali.

Bisimba amesema pamoja na hayo yote anamshauri Rais Magufuli kuangalia sana kwenye upande wa utawala wa sheria na kufuata misingi ya katiba kwa kila jambo analolifanya kwasababu hadi sasa mambo anayoyafanya ni mazuri sana, hivyo asipo kwa mujibu wa sheria ataharibu kizuri alichofanya.

Amesema Rais Magufuli asizuie siasa kwani anajua kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria bali afuatilie kuona kwamba zinafanyika kwa njia ambayo itajenga badala ya njia ambayo itabomoa. Bofya hapa kutazama video

Juan Mata Athibitisha Kwa Vitendo, Mourinho Amkubali
Stephane Sessegnon Arejea Ufaransa