Klabu ya Montpellier inayoshirikis ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa (Ligue 1) imemsajili aliyekua kiungo mshambuliaji wa  West Bromwich Albion Stephane Sessegnon.

Montpellier wamekamilisha mpango wa usajili wa kiungo huyo kutoka nchini Benin kwa mkataba wa miaka miwili.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, ameelekea nchini Ufaransa akiwa kama mchezaji huru kufuatia kauchwa na klabu West Brom mwishoni mwa msimu uliopita.

Hii si mara ya kwanza kwa Sessegnon, kuwa sehemu ya wachezaji wa klabu za nchini Ufaransa, kwani aliwahi kufanya hivyo akiwa na Paris St Germain kabla hajatimkia Uingereza kujiunga na Sunderland, na baadae alikwenda West Brom.

Video: Dk. Kijo Bisimba amshauri Rais JPM kufuata misingi ya katiba, utawala wa sheria
Jack Wilshere Amuweka Njia Panda Mwenyekiti Wa Bournemouth