Rapa Eminem amemkosoa vikali rais Donald Trump kwenye video iliyooneshwa kwenye tamasha la BET la tuzo za Hip-Hop kwa kumuita Trump babu mwenye miaka 94 mbaguzi wa rangi.

Eminem pia amewakosoa wanao muunga mkono huku akimuita rais Trump mtu asiyejali mambo ya msingi ya wamarekani.

Rapa huyo ambaye anatimiza miaka 45 tarehe 17 mwezi Octoba mwaka huu anatarajia kutoa albamu yake mpya tarehe 17 mwezi Novemba 2017 ambayo itakuwa albamu ya tisa tangu alipoachia The Marshall Mathers LP 2   mwaka 2013.

Tazama video hiyo ya Eminem akimchana rais Donald Trump hapa chini;

Hii sio mara ya kwanza kwa rais Trump kutukanwa na wanamuziki nchini Marekani kwani mapema mwezi Agosti rapa YG kutoka Califonia aliachia wimbo wa kumchana Trump unaoitwa ‘FDT’, wimbo ambao tafsiri yake ni matusi makali.

Mvua zasababisha maafa Tabora
Australia yadukuliwa siri za kijeshi