Je unafahamu kuwa mtoto chini ya miezi 6 anatakiwa kupewa maziwa ya mama peke yake, japokuwa wamama wengi huona maziwa ya mama pekee hayajitoshelezi kufanya mtoto ashibe hivyo humuongezea na chakula cha ziada.
Mtoto akishafikisha miezi sita anatakiwa kupewa maziwa ya mama pamaoja na vyakula vingine, na mtoto anatakiwa kunyonya maziwa ya mama hadi atakapofikisha miaka miwili au zaidi.
Dar24Media ilifanya mahojiano na Afisa Mtafiti masuala ya Lishe kutoka TFNC, Doris Kitana kupitia kipindi cha Afya Tips, amesema mtoto anapokuwa analishwa haishauriwi wala kutakiwa kumkaba mtoto ili kumfanya ale chakula kwani njia hiyo inaweza kumfanya mtoto aweze kukabwa au kupaliwa na chakula.
Aidha moja ya wanasaikolojia waligundua kwamba mtoto aliye na njaa hukunja ngumi huku mtoto aliyeshiba huachia ngumi yake, watoto wengi wamekuwa na tabia hiyo ambapo wazazi au walezi wamekuwa hawafahamu tafsiri ya ishara hiyo inayooneshwa na mtoto pindi anapolishwa au akiwa na njaa.
Tazama Video zaidi hapa chini.