Muigizaji maarufu kutoka nchini Kenya Lupita Nyong’o ameweka rekodi nyingine kwenye mauzo ya filamu mpya ya US iliyoachiwa rasmi Machi 8,2019, baada ya kufanya vizuri kwenye filamu ya Black Panther iliyotoka Februari mwaka jana.
Katika filamu hiyo mpya Lupita amecheza kama Mhusika mkuu (Main Character), imeweza kuingiza jumla ya dola za Kimarekani 70.2 millioni sawa na bilioni 165 za Kitanzania.
Aidha filamu hiyo imevuka lengo la makisio ambapo ilitabiriwa kuingiza kiasi cha ($68 millioni) sawa na Tsh bllioni 159 kabla haijatoka.
Imeelezwa kuwa filamu ya US imeongozwa na kuandikwa na Jordan Peele, iliachiwa kwa mfumo wa Trailer na ilitengenezwa kwa bajeti ya dola millioni 20 za kimarekani sawa na Zaidi ya billioni 46 za kitanzania.
Kutokana na mauzo hayo filamu ya US inatajwa kuwa filamu ya kutisha iliyouza Zaidi Dunianai kwenye wiki ya kwaza kwa muda wote
[youtube https://www.youtube.com/watch?v=1tzFRIQfwXg]