Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee na kumuweka ndani kwa saa 48 kwa madai ya kutoa kauli za uchochezi wakati akizungumza na waandishi wa habari jana Julai 3, 2017.

Mbunge huyo anadaiwa kutoa kauli za kichochezi wakati akizungumza na Waandishi wa habari Makao Makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambapo Hapi ameagiza Mbunge huyo akamatwe mara moja na kuwekwa rumande ili atoe ushirikiano kwa jeshi la Polisi kuhusu kauli hizo.

Vichwa vya treni vyazua utata bandarini, TRL yakana kuvimiliki
Deogratius Munishi ‘Dida’ Atemwa Young Africans