Tanazania itaanza kuuza madini ya TIN yanayopatikana mkoani Kagera mwishoni mwa mwezi November mara baada ya kupata cheti cha kuruhusu kufanya hivyo na kufanya kuongezeka kwa thamani ya madini hayo na kuongeza pato la Taifa.
Hayo yamesemwa na waziri wa madini Mhe Dotto Biteko wakati wa ziara yake mkoani Kagera alipokuwa akizindua jengo la kituo cha umahili (Centers of Excellence) lililojengwa manispaa ya Bukoba, ambapo amesema kuwa serikali ya Tanzania pamoja na kuwa na madini ya TIN ilikuwa haina kibali cha kuuza madini hayo nje ya nchi,…Bofya hapa kutazama