Mku wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amefanya ziara ya kukagua wajasiriamali wadogo wenye vitambulisho vya ujasirimali katika Soko la Kariakoo Jijini Dar es salaam ambapo amewaonya Wamachinga wanaoghushi vitambulisho ili wakwepe gharama.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa mpaka sasa vilikuwa vimebaki vitambulisho, 3000 baada ya kugaiwa kwa wakuu wa Wilaya.
“Masikitiko yangu Wamachinga wamekuwa sio waaminifu, kwasababu wamekuwa wakivitoa copy hivyo ili wasilipe 20000, na wanakuwa na vitambulisho feki ni kosa kisheria kuchukua nyaraka ya Serikali kukitoa kopi,” amesema Makonda.
Aidha, Makonda amesema kuwa wamegundua katika watu 10, ni watu 4 tu ambao hawana vitambulisho, huku akiwataka wakuu wa Wilaya kufanya msako kwa wafanyabiashara ambao watakuwa hawana vitambulisho.