Mgombea Urais wa chama cha Republican Marekani, Donald Trump amekatishwa kutoa hotuba yake baada ya kumshutumu mpinzani wake Hillary Clinton.

Hotuba ya Trump imekatishwa na Mchungaji, Faith Green Timmons wa Kanisa la Bethel United Methodist la Wamarekani weusi katika jimbo la Michigan.

Trump alikatishwa hotuba hiyo baada ya kumshutumu mgombea huyo wa chama cha Democratic, Clinton kuhusu mikataba ya kibiashara duniani.

“Trump, nilikualika hapa uje kutushukuru kwa juhudi ambazo tumefanya Flint, si kutoa hotuba ya kisiasa,” – Mchungaji, Faith Green Timmons

Baada ya hayo Trump aliendelea na kuzungumzia kwa kifupi kuhusu kutatua matatizo ya maji safi Flint lakini aliambulia kuzomewa na baadhi ya watu kwenye umati huo hali iliyopelekea mgombea huyo kulazimika kukatiza ghafla hotuba yake, ambayo imedumu kwa dakika sita hivi.

Walimu wagoma kukatwa mshahara kununua sare za Mwenge wa Uhuru
Bodi ya mikopo yawatendea haki wanafunzi wa elimu ya juu kwa mara ya pili.