Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro leo amekutana na waandishi wa habari ofisini kwake na ametoa taarifa za kukamatwa kwa mtu mmoja anayetuhumiwa kwa kuuza fulana zenye maneno yanayodaiwa kuwa ni yakichochezi.

Sirro amesema kuwa Jeshi hilo la Polisi lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa maeneo ya Kinondoni kuna duka linauza flana zenye maneno ya uchochezi yaliyoandikwa ‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’, ‘UKUTA’ 

Aidha, Kamanda Sirro amesema kuwa wapo watu wanaosema kwanini wanafanya mazoezi, ambapo Sirro ameeleza kuwa Jeshi la Polisi ni kawaida kufanya hivyo na pia jeshi hilo linafanya maandalizi kwa wanaotaka kuvunja sheria.

Bofya hapa kutazama video #USIPITWE

Simon Sirro – Huu Ukuta utabomoka tu, kwa Dar es salaam umeshabomoka

A video posted by Dar24 (@dar24news) on

FIFA Yawaongezea Ujuzi Makocha Tanzania
Jeshi la Polisi latolea majibu picha za askari wakifanya mazoezi