Sakata la Kesi ya Chama cha Wananchi CUF iliyofunguliwa na wanachama wanao muunga mkono Maalim Sharrif Hamad dhidi ya bodi ya wadhamini ya chama hicho inayotambuliwa na Lipumba imeahirishwa mpaka tarehe 11 Agosti mwaka huu.

Kesi hiyo iliyofunguliwa na mbunge wa mbunge wa Malindi, Ally Saleh (CUF) inapinga kugsajiliwa kwa bodi ya wadhamini iliyopo upande wa Lipumba na kuwa hukumu itakayotolewa ndio itatoa maamuzi kuwa ni CUF ipi ambayo inapaswa kuwepo.

Hayo yamesemwa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Wabunge CUF, Riziki Ngwari mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, ambapo amesema kuwa hukumu itakayotolewa itaamua kuwa CUF ipi ambayo ina haki yakuwepo na kuendelea na shughuli za chama.

Magazeti ya Tanzania leo Julai 22, 2017
Video: Mwanasheria wa Tundu Lissu agonga mwamba, ashindwa kuonana na mteja wake