Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa Menyekiti wa chama hicho ambaye anatambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba si mwanachama wa chama hicho.

Maalim Seif amesema hayo leo Juni 28, 2017 jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa hawezi kukaa meza moja na Mwenyekiti huyo aliyejiuzuru.

“Mimi siwezi kukaa meza moja na Prof. Lipumba, kwanza siyo mwanachama wetu na alishajiuzuru kwenye nafasi yake aliyokuwa nayo, hivyo siwezi kuzungumza naye chochote masuala ya chama,”amesema Maalim Seif.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kutokana na fujo alizozifanya katika mkutano mkuu wa taifa wa chama hicho, Baraza`Kuu lilimfukuza uanachama hivyo hana nafasi yeyote ndani ya CUF.

Magazeti ya Tanzania leo Juni 29, 2017
Kigoma kujengewa Mahakama Kuu