Waziri Mkuu aliyejiuzuru, Edward Lowassa amesema kuwa amesikitishwa sana na kitendo cha Serikali ya Mkoa wa Dar es salaam ya kuzuia kongamano la kisiasa lililokuwa limeandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Ilala.

Lowassa amesema kuwa kila chama cha siasa hapa nchini kina haki ya kufanya shughuli zake za kisiasa bila kuingiliwa na mhimili wowote hivyo kuzuia kongamano hilo ni kuwanyima haki wanachama wa chama husika.

“Lengo la kongamano hili lilikuwa ni kuwaleta pamoja watu kuweza kujadili siasa za ushindani na Demokrasia ya kweli, tofauti zetu zisitutenganishe tushindane kwa hoja maana kwa sasa imetokea dhana ya kwamba wanachadema ni wavuruga amani,”amesema Lowassa.

Aidha, katika hatua nyingine Lowassa amesema kuwa, Rais Dkt. Magufuli alipaswa kwenda Arusha mara baada ya kutokea kwa ajali iliyosababisha wanafunzi 32 waalimu wawili na dereva wa gari la shule ya Luck Vincet.

Hata hivyo, amekikumbusha Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa kisitarajiwe kuwa kitaendelea kuwa madarakani siku zote, hivyo wasijisahau katika maamuzi yao wanayofanya kwani nchi hii ni ya wote.

Fainali za AFCON U-17 kuanza kutimua vumbi leo
NEC kulitengea bajeti daftari la wapiga kura