Aliyekuwa Naibu Waziri wa fedha katika utawala wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Adam Kighoma Malima leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na tuhuma za kuwazuia Polisi kufanya kazi yao.

Katika kesi hiyo ambayo mlalamikanji ni Askari H.7818 PC Abdul, Adam Malima anashitakiwa kufuatia tukio lililotokea jana maeneo ya Masaki jirani na Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam.

Katika madai yake, PC Abdul anasema yeye akiwa na askari wenzake na maafisa wa Kampuni ya PBELinayojihusisha na kukamata watu wanaopaki magari hovyo, wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao, walizuiwa kutekeleza majukumu yao na naibu waziri huyo mstaafu akishirikiana na wananchi waliokusanyika mahali hapo.

“Kufuatia hali iliyokuwepo kwenye eneo hilo, niliamua kupiga risasi sita hewani ili kuwatuliza watu waliokuwa wanazomea wakiongozwa na mtuhumiwa,” alisema PC Abdul.

Mahakama imemwachilia huru Malima kwa dhamana ya shilingi milioni tano

Magazeti ya Tanzania leo Mei 17, 2017
Video: Sirro azungumza kuhusu Askari aliyepiga risasi hewani