Kamishana wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amezungumza kuhusu tukio lililotokea Mei 15, 2017 la Askari Polisi kupiga risasi hewani wakati akijibizana kwa maneno na Naibu Waziri wa zamani wa Fedha, Adam Malima.

Kamishna Sirro amesema kuwa tukio hilo limetokea baada ya dereva wa gari la Malima pamoja na Malima mwenyewe kukutaa kutii amri halali ya Askari Polisi. Amesema kitendo cha Askari hao kupiga risasi hewani ni kutokana na mazingira pia kama Askari hao wangeshindwa kufuata kanuni na maelekezo wangeshtakiwa wao kwani vielelezo vipo.

Tukio hilo lilitokea katika eneo la Masaki jijini Dar es salaam ambapo dereva wa Malima alikuwa ameegesha gari vibaya ambapo alijibizana na Kampuni ya Udalali ya Majembe kabla ya polisi kuingilia kati na kufyatua risasi hewani.

Amesema Malima pamoja na dereva wake wamelala mahabusu na leo wamepelekwa mahakamani kujibu tuhuma. Tazama hapa video

Video: Maamuzi ya Mahakama kuhusu Adam Malima
P-Funk aeleza rapa wa Marekani MIMS alivyompa jina la kundi lake ‘Bongolos’