Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), limeagizwa kuanza kufanya tathmini ya kisayansi kuhusu manufaa ya Mifuko yote ya uwekezaji nchini ili kujiridhisha endapo inawanufaisha wananchi kama ilivyokusudiwa.

Agizo hilo leo Aprili 18, 2017 wakati akifungua maonesho ya mifuko ya uwezeshaji katika uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma ambapo pia amelitaka baraza hilo kufanya tathmini kuhusu namna ya kuunganisha mifuko hiyo bila ya kuathiri majukumu ya msingi na mantiki ya kuanzishwa kwake, ili inayofanya kazi zinazofanana iunganishwe.

Majaliwa amesema uzinduzi wa maonesho hayo ni fursa nzuri kwa wananchi kuweza kudadisi kuhusu huduma zitolewazo na Mifuko hiyo na kutoa ushauri, ili kuboresha huduma.

“Lengo ni kuwa na Mifuko michache, lakini inayobadilisha maisha ya wanufaika, ambao ni wananchi. Nitafurahi kupata taarifa hiyo kabla au ifikapo Mwezi Mei, 2018,” amesema Majaliwa.

Majaliwa amesema mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi yanayofanywa na Serikali yanalenga kuwawezesha Watanzania wengi wafanye  shughuli za kujiongezea kipato bila kusumbuliwa na baadhi ya Watumishi wasio waadilifu.

“Uwezeshaji wananchi kiuchumi ni jambo ambalo lipo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/2017 – 2020/2021,”.

Aidha, Kabla ya Waziri Mkuu kutoa agizo hilo, Katibu Mtendaji wa NEEC, amesema maonesho hayo ya siku nne yatawezesha kuwaongezea wananchi uelewa juu ya shughuli zinazofanywa na mifuko ya uwezeshaji.

 

Video: Kendrick Lamar aachia video ya ‘DNA’ kutoka kwenye DAMN
Tanzia: Baba mzazi wa msanii Belle 9 afariki dunia